Netflix kuendeleza Orange is the New Black

Uzo Aduba Haki miliki ya picha EPA
Image caption Uzo Aduba ameshinda tuzo mbili za Emmy

Mashabiki wa kipindi cha runinga cha Orange is the New Black wana sababu ya kutabasamu kwani kipindi hicho kitaendelea, kwa misimu mingine minne.

Netflix wamethibitisha kwamba wameidhinisha kuandaliwa kwa misimu mitatu, juu ya msimu wa nne ambao unatarajiwa kuanza kupeperushwa mwezi Juni.

Mwandalizi wake, Jenji Kohan, pia ametia saini mkataba wa kuendelea kuandaa vipindi hivyo hadi msimu was aba.

Kipindi hicho, ambacho huangazia maisha ya wanawake gerezani, kilishinda tuzo ya kipindi bora cha ucheshi katika Tuzo za Chama cha Waigizaji mwaka huu.

Mmoja wa waigizaji wake Uzo Aduba ameshinda tuzo mbili za Emmy kutokana na uigizaji wake kwenye filamu hiyo.

“Miaka mingine mitatu! Si muhula wa uongozi, lakini ni muda wa kutosha kufanya ammbo ya kuvutia. Katika baadhi ya tamaduni, “nakutakia maisha yenye msisimko,” huwa ni laana, lakini mimi siishi katika tamaduni hizo. Hapa, kuwa na msisimko ni kuwa na msisimko," amesema Jenji Kohan baada ya tangazo la Netflix.