Kilemba chamzuia Kalasinga kupanda ndege

Image caption Kalasinga

Msanii mmoja wa Kikalasinga amedai kwamba alizuiwa kupanda ndege kutokana na kilemba chake.

Nyota huyo wa India-American,Waris Ahluwalia,ambaye pia ni mwanamitindo amesema kuwa alikatazwa kupanda ndege hiyo alipokataa kutoa kilemba chake hadharani.

Kisa hicho kilitokea wakati wa ukaguzi wa kiusalama kabla ya kuondoka kwa ndege kutoka mjini Mexico hadi New York.

Kampuni ya ndege ya Aeromexico imesema kuwa imeafikia itifaki za kiusalama na inajuta kwa kisa hicho.

Image caption Kalasinga

Alichapisha picha ya tiketi yake katika mtandao wa akaunti yake ya Instagram.Ilikuwa na muhuri ulioandikwa ''SSSS'' ambao huwachagua abiria ili kufanyiwa ukaguzi zaidi.

Ukaguzi huo hufanywa bila kuchagua.

Bwana Ahluwalia,ambaye alionekana katika hoteli ya Grand Budapest na kushiriki katika kampeni ya chapa cha nguo za Marekani ya GAP alisema kuwa alikuwa akielekea kushiriki katika hafla ya wanamitindo ya New York Fashion Week.

Image caption Kalasinga

Katika mahojiano na gazeti la the New York,Bwana Ahluwalia alisema aliafikia ukaguzi wa ziada lakini akakataa kutoa kilemba chake alipoulizwa na maafisa wa ndege hiyo kufanya hivyo.

''Hicho si kitu ambacho ningefanya hadharani'',alinukuliwa akisema.''Hiyo ni sawa na kumwambia mtu avue nguo zake''.