UAE yaunda wizara mpya ya 'furaha'

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum,Kiongozi wa UAE ,

Waziri mkuu wa Miliki za Kiarabu UAE ametangaza kuundwa kwa wizara mpya ya furaha.

Wizara hiyo mpya imeundwa katika mabadiliko yaliyotekelezwa na utawala wa kiongozi wa UAE Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum.

Sheikh Maktoum, ambaye ni kiongozi wa Dubai amesema wizara hiyo mpya furaha inaazimia ''kuchochea mtagusano baina ya wananchi wake mbali na kuhamasisha umma utosheke na kile walichonacho''.

Wizara mpya nyingine iliyoundwa ni ''wizara ya kuvumiliana''.

Sheikh Maktoum vilevile ameagiza kuunganishwa kwa wizara nyingi mbali na kutoa zabuni za kuagiza makampuni kutoka nje kuendesha asilimia kubwa ya shughuli za serikali.

"Serikali sharti iweze kunyumbulika kwa urahisi. Nafkiiri hatuitaji wizara zaidi tunachoitaji ni mawaziri wenye uwezo wa kutafsiri mabadiliko na kuatekeleza ipasavyo'' Sheikh Makhtoum aliiambia kongamano la dunia linalojadili miundo ya utawala na serikali mjini Dubai.

''Tunachotaka ni serikali changa itakayokidhi matakwa ya vijanana uma.''

Wizara ya uvumilivu inanuiwa kupalilia nguzo muhimu ya jamii ya raia wa miliki za kiarabu '' alisema Sheikh Makhtoum kupitia mtandao wake wa Tweeter.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wizara ya vijana nayo itaongozwa na waziri mwanamke ambaye umri wake hautazidi miaka 22.

Vijana pia hawakusaulika aliunda baraza la vijana la taifa ''Youth National Council''.

Wajibu wao mkubwa ni kuishauri serikali kuhusiana na maswala yanayowahusu vijana na wataongozwa na waziri mwanamke ambaye umri wake hautazidi miaka 22.

''Vijana ndio utawala ujao wa taifa hili '' aliongozea.