Mwaka wa neema wa Kanisa

Haki miliki ya picha Reuters

Zaidi ya mapadre na watawa elfu moja waliopewa wadhifa wa kutakasa na kutoa msamaha wa dhambi ambazo huwa ni baba mtakatifu pekee anayetoa msamaha,wameanza hija ya kueneza neno la Mungu kwa kutembelea maeneo mbalimbali ulimwenguni ikiwa ni miongoni mwa malengo yaliyowekwa katika kuadhimisha mwaka wa neema wa kanisa.

Wamisionari hao waliyochaguliwa na Papa Francis wamepewa nadhiri ya kwenda mbali na katika eneo kubwa zaidi,na miongoni mwa mipango iliyopo ni kufika Australia kwa usafiri wa gari na ziara nyingine ni katika ya kijamii ya Canada .