Korea Kusini yavunja ushirikiano na korea Kaskazini

Kaesong Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kiwanda cha Kaesong ambacho shughuli zake zitaathirika

Korea kusini imesitisha harakati zake kwenye kiwanda inachoendesha pamoja na Korea Kaskazini kufuatia hatua ya hivi karibuni ya korea kaskazini ya kuzindua mpango wake wa roketi na majaribio ya nukilia.

Utawala wa mjini Seoul umesema kuwa shughuli zake katika kiwanda hicho zitavunjwa, ili kuizuia korea kaskazini kutumia uwekezaji wake " katika kufadhili mpango wa wa nukliana kutengeneza makombora".

Kaesong ni kituo cha mwisho cha ushirikiano baina ya nchi hizo mbilii na ni chanzo muhimu cha mapato ya Pyongyang.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais wa Korea kaskazini Kim Jong Un akishuhudia kurushwa kwa roketi mwezi Januari

Hii inakuja huku Japan ikiweka vikwazo vipya dhidi ya Korea kaskazini kufuatia uzinduzi wake wa nuklia.

Vikwazo hivyo ni pamoja na kupiga marufuku vyombo vyote vya baharini bya Korea kaskazini kuingia kwenye bandari yoyote nchini Japan na pia vile vinavyotoka nchi nyingine vilivyotembelea taifa hilo.

Jana Marekani ilionya kwamba Korea kaskazini inaweza kuwa na The US warned on Tuesday that the North could soon have enough plutonium sumu ya madini ya Plotonium ya kutosha kuweza kutengeneza silaha za nuklia .

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Taarifa ya kurushwa kwa roketi angani i Januari ilizusha wasi wasi mkubwa duniani

Korea Kusini, Marekani , Japan na wengine wanaonelea hatua ya Jumapili ya uzinduzi wa roketi kama njia ya Korea kaskazini ya kuweka setilaiti angani - kama njia ya kuficha teknolojia iliyopigwa marufuku ya majaribio ya makombora.

Hali ya wasi wasi imetanda katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita tangu Korea Kaskazini ilipofanya majaribio manne ya Nuklia mapema mwezi Januari.