Msikiti wa Muammar al-Gaddafi Kampala

Image caption Msikiti wa Muammar al-Gaddafi mjini Kampala Uganda

Ukiwa ni mgeni mjini Kampala Uganda jengo linalokukaribisha ukitizama eneo la mashariki mwa mji huo ni msikiti wenye rangi ya hudhurungi.

Msikiti huo ulianzishwa na rais wa zamani generali Idi Amin Dada.

Katika eneo la Old Kampala msikiti huo ndio unaohudumia maelfu ya wakazi.

Msikiti huo ndio moja ya misikiti mikubwa zaidi kusini mwa jangwa la Sahara.

Msikiti huo ulioanzishwa ujenzi wake yapata miaka 30 iliyopita, unafahamika kama msikiti wa Muammar al-Gaddafi.

Image caption Rais Gaddafi wa Libya ndiye aliyechangia fedha za kuukamilisha msikiti huo mkubwa

Je utauliza unaitwaje msikiti wa kiongozi huyo wa Libya?

Ni kwa sababu marehemu rais huyo wa Libya ndiye aliyechangia fedha za kuukamilisha msikiti huo mkubwa.

Msikiti huo unauwezo wa kuwabeba takriban waumini 15,000 katika ibaada .

Alipozuru Libya na kuufungua rasmi msikiti huo ,marehemu kiongozi wa Libya, Muammar al-Gaddafi maelfu ya waumini wa kiislamu nchini humo walishangilia na kumtakia maisha marefu kwa kukamilisha ndoto ya rais wa zamani wa Uganda Idi Amin Dada.

Image caption Msikiti huo unauwezo wa kuwabeba takriban waumini 15,000 katika ibaada .

Wakati huo rais Amin alikuwa akiishi uhamishoni alikokimbilia baada ya mapinduzi yaliyoongozwa na aliyekuwa rais Milton Obote, mwaka wa 1979.

Viongozi wengine wa Afrika walihudhuria hafla hiyo akiwemo rais wa Somalia Zanzibar na Djibouti.

Sheikh wa msikiti huo Hajj Nsereko Mutumba anakiri kuwa rais huyo wa zamani japo alituhumiwa kwa mauaji ya maelfu ya wapinzani wake pia alichangia pakubwa ukuaji wa dini ya Kiislamu nchini Uganda.