Babu 94, ashtakiwa kwa mauaji ya wayahudi laki moja

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mlinzi wa zamani wa utawala wa Nazi amefikishwa mahakamani nchini Ujerumani kwa kuhusika kwa mauwaji ya watu 170,000

Mlinzi wa zamani wa utawala wa Nazi amefikishwa mahakamani nchini Ujerumani kwa kuhusika kwa mauwaji ya watu 170,000 katika kambi ya mauwaji ya wayahudi Auschwitz.

Reinhold Hanning mwenye umri wa miaka 94 ni mmojawepo wa waliokuwa walinzi wa utawala wa Nazi ambaye angali hai.

Sajini huyo mkuu amesisitiza kuwa katika kipindi chote alichohudumu katika kambi hiyo hakuna mauaji yaliyofanyika.

Serikali kupitia kwa mkuu wa mashtaka ya umma inashikilia kuwa mauaji hayo ya kihistoria hayangefanyika kusingekuwepo na walinzi waliotekeleza amri ya Nazi.

Aidha ''Hungarian action ya 1944''kama operesheni hiyo ya mauaji ilivyoitwa ilifanikishwa na mamia ya walinzi waliotekeleza masharti makali ya kuwazuia wayahudi hao mateka wasitoroke kizuizini.

Haki miliki ya picha Georgiy Ugrynovych
Image caption Amekanusha kuhusika na mauwaji ya halaiki ya mwaka wa 1944

Waendesha mashtaka wanaamini kuwa alikutana na wafungwa wa kiyahudi walipofika katika kambi hiyo na kuna uwezekanao aliwapeleka wengi wao ndani ya kichumba cha gesi ya mauti.

Amekanusha kuhusika na mauwaji ya halaiki.

Schwarzbaum mwenye umri wa miaka 94 alipelekwa kwenye kambi hiyo ya Auschwitz 1943.

Kesi hiyo inafwata mfano wa kesi ya kwanza dhidi ya John Demjanjuk mwenyeji wa Ohio alipatikana na hatia ya kufanikisha mauaji ya halaiki ya wayahudi.

Jopo la kisheria la kusikiza kesi ya aina hiyo liliundwa mnamo mwaka 2011 nchini Ujerumani, pale mahakama ilipompata na hatia mlinzi mwingine wa uliokuwa utawala wa NAZI Ivan Demjanjuk ya mauwaji ya halaiki.