Palestina yatoa wito wa msaada wa chakula

Image caption Palestina yatoa wito wa msaada wa chakula

Serikali ya Palestina na Umoja wa Mataifa zimetoa wito wa pamoja wa ufadhili zaidi huku uhasama kati ya Palestina na Israeli ukiendelea kutokota.

Palestina na Umoja wa Mataifa zinatarajiwa kuchangisha dola milioni mia tano.

Ghasia na machafuko ya hivi karibuni zimesababisha vifo vya zaidi ya raia mia mbili wa Palsetina.

Wengi wao wanatuhumiwa na Israeli kwa kufanya mashambulio dhidi yake.

Msaada ulioombwa kwa mwaka huu utatumiwa kwa minajili ya chakula kwa karibu watu millioni 1.6 wanaohitaji msaada katika utawala wa Palestina ambao ni thuluthi moja ya watu wote katika ukingo wa Magharibi na Gaza.

Afisa mmoja wa kipalestina alionya kuwa uhaba wowote utasababisha hali ambayo tayari sio nzuri kulipuka.

Image caption Palestina na Umoja wa Mataifa zinatarajiwa kuchangisha dola milioni mia tano.

Mwaka 2015 ni nusu tu ya fedha zilizoombwa na umoja wa mataifa zilipatikana ambapo wengi walikosoa hatua ya kupeleka fedha kufanya miradi mingine eneo la mashariki ya kati

Baadhi ya wataalamu wa kimataifa wamesema kwa kuongezeka kwa mashambulizi dhidi ya Israeli miezi michache iliyopita huenda yakavuruga kutolewa kwa misaada hiyo.

Wapalestina wanasema kwa kushindwa kwa mazungumzo ya amani kumaliza hatua ya Israeli kudhibiti maeneo takatifu ndiko kumechochea ghasia zinazoendelea.

Israeli nayo inalaumu viongozi wa wapalestina na mitandao ya kijamii kwa uchochezi.