Kijana aliyetegua kitendawili cha Kanye West

Kanye Haki miliki ya picha
Image caption Kanye West ametoa albamu mpya

Kijana mmoja nchini nchini Marekani anatarajia zawadi kutoka kwa mwanamuziki Kanye West baada yake kufanikiwa kujibu swali lake.

Dante Holley, 20, alifanikiwa kueleza kwa kirefu herufi TLOP zinasimamia nini kwenye jina la albamu ya mwanamuziki huyo ulio ambalo limetolewa kutoka kwa wimbo wake mpya kwa jina No More Parties in LA.

Atapokea tiketi za kuhudhuria maonyesho ya mavazi ya Kanye West ya Yeezy makala ya tatu, pamoja na mavazi yenyewe.

Iwapo bado unatafakari zinasimamia nini, zinasimamia The Life of Pablo.

"Alikuwa akizungumzia alivyohisi kama Pablo alipokuwa akishughulikia viatu vyake, alijihisi kama alivyohisi Pablo alipokuwa akiangaziwa kwenye habari,” ameambia BBC.

"Nilifikiria kwamba alikuwa anazungumzia Pablo Escobar au Pablo Picasso.

"Kwa hivyo nikafikiria lazima iwe The Life of Pablo."

Dante anatoka New Jersey nchini Marekani na ni mwanarepa na produsa wa muziki. Anafanya kazi na HW4L Records.

Alifrahi sana alipogundua kwamba alikuwa amepata swali hilo kuhusu TLOP.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kanye West pia hutengenza na kuuza mavazi

"Simu yangu ilianza kuita. Nilifikiria Kanye alikuwa ametangaza jina kamili na lilikuwa The Life of Pablo," anakumbuka.

"Watu walinipigia kila mmoja akiniambia, 'Umeshinda, umeshinda’. Nilifurahi sana. Singetarajia hilo.”

Dante anasema wahudumu wa Kanye hawajawasiliana naye bado.

Lakini atatumia zawadi hiyo kusaidia watu wasiojiweza.