Madaktari wapinga uhamisho wa mtoto Australia

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Australia

Mamia ya watu wamekusanyika katika hospitali moja nchini Australia kuwaunga mkono madaktari ambao wamekataa kumuachilia mtoto msichana ambaye huenda akaondelewa nchini humo.

Madaktari wanasema kuwa mtoto huyo hawezi kuondolewa hadi pale makao bora yatakapopatikana.

Alipatwa na ajali mbaya ya moto katika kituo kimoja cha wahamiaji kilichopo katika kisiwa cha Nauru.

Sera za Australia za kuwazuia wahamiaji kwenye vituo vilivyo nje ya nchi hiyo imekashifiwa pakubwa lakini serikali inasema kuwa ni muhimu kuwazuia watu kusafiri kwenda Australia wakitumia mashua mbovu.