Papa Francis aomba wakristo kulindwa

Haki miliki ya picha AP
Image caption Papa Francis na mkuu wa kanisa la Orthodoz nchini Urusi Patriach Kirill

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani na mkuu wa kanisa la Orthodox nchini Urusi wamefanya mkutano wao wa kwanza baada ya takriban miaka 1000 tangu kuwepo kwa mgawanyiko kati ya makanisa hayo mawili pande za magharibi na mashariki.

Baada ya mazungumzo yalioyofanyika nchini Cuba Papa Franciss alisema kuwa walikuwa wamezungumza kwa njia iliyo wazi na watatafuta njia za kufanya kazi kwa pamoja huku mkuu wa kanisa la Orthodox la Urusi Patriarch Kirill akisme kuwa nia yao ni kulinda ukiristo kote duniani.

Katika taarifa ya pamoja wawili hao wametoa ombi la kulindwa kwa wakristo wanaoshambuliwa Syria na mashariki ya kati.

Wakiwanyoshea kidole cha lawama wapiganaji wa Jihadi,walisema kuwa familia za jamii hiyo zinaangamizwa huku kumbukumbu za kidini zikiharibiwa.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Papa Francis na Kirill

Pia wamesema kuwa msaada wa kibinaadamu unahitajika ili kuwashughulikia wakimbizi wanaotoroka Syria na Iraq.

Patriarch Kirill ambaye ni mshirika mkuu wa rais wa Urusi Vladimir Putin aliyeandaa mkutano huo na waandishi wa habari ameongezea kuwa bwana Putin anatafuta washirika wakati kuna msukosuko katika maeneo mengi ya dunia.