Hewa chafu husababisha vifo milioni 5.5 duniani

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Hewa chafu nchini Uchina

Utafiti mpya umeonyesha kuwa watu milioni tano unusu kote duniani wanakufa kila mwaka kutokana kuchafuka kwa mazingira.

Zaidi ya nusu ya watu waliokufa wanaripotiwa kutoka nchini China na India ambapo ukuaji wa uchumi umechangia uchafuzi mkubwa wa hewa.

Viwanda, magari na uchomaji wa makaa ya moto ndivyo vimechangia zaidi.

Kupumua hewa iliyochafuka husababisha magonjwa ya kupumua na saratani ya mapafu.