Syria:Marekani yasema Assad anajidanganya

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mapiganao nchini Syria

Marekani inasema kuwa rais wa Syria Bashar al-Assad anajidanganya ikiwa anaamini kuwa kuna suluhu la kijeshi kwa mzozo ulio nchini mwake.

Wakati wa mahojiano ya siku ya Ijumaa, Assad alitangaza wazi mipango yake ya kuendelea kupigana hadi pale taifa lote la Syria litakapoingia mikononi mwake.

Lakini msemaji wa wizara ya mashauri ya kigeni nchini Marekani alisema kuwa mipango ya Assad italeta umwagikaji zaidi wa damu.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption rais Bashar al Assad

Wakati huo huo viongozi wa dunia wanaokutana mjini Munich wameafikia makubaliano yenye lengo la kumaliza ukatili nchini Syria ndani ya wiki moja.

Lakini makundi ya waasi yanasema kuwa hayataweka silaha chini hadi Urusi iache kuwashambulia na kuhakikishiwa kuwa Assad ataondolewa madarakani.