Mauaji ya raia Syria:Urusi yashutumiwa

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mabomu ya Urusi

Waziri mkuu wa Ufaransa, Manuel Valls, amesema kuwa Urusi lazima iache kuwarushia mabomu raia wa Syria, ili kuweza kurejesha amani.

Alisema hayo katika mkutano wa viongozi wa mataifa kadha mjini Munich, siku moja baada ya kufikia makubaliano ya kujaribu kumaliza mapigano nchini Syria.

"Ufaransa inaiheshimu Urusi na masilahi ya Urusi.Ma-rais wetu wanazungumza mara kwa mara.Lakini tunajua, kuwa ili kufikia tena njia ya kurejesha amani na majadiliano, basi Urusi lazima iache kutupa mabomu maeneo ya raia''.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Manuel Valls

Urusi imesema hakuna ushahidi kuwa mashambulio ya ndege yanadhuru raia.

Hapo awali, Marekani ilisema rais wa Syria, Bashar al-Assad, anajidanganya, ikiwa anafikiri kuwa hatua za kijeshi zitaleta suluhu, katika vita vya nchini mwake.