Awamu ya pili ya uchaguzi yafanyika CAR

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Uchaguzi CAR

Raia wa taifa la jamhuri ya Afrika ya kati wanapiga kura hii leo kwa awamu ya pili ya uchaguzi huo wa urais na ule wa ubunge uliofanyika mwezi Disemba ambao ulisitishwa kutokana na udanganyifu.

Uchaguzi huo unaonekana kuwa hatua ya kuleta amani ,uthabiti na serikali ya kidemokrasia baada ya wapiganaji wa kiislamu kuchukua mamlaka mwaka 2013 na kusababisha vita na wapiganaji wa kikristo.

Wagombea wote wa urais ,aliyekuwa waziri mkuu Faustin Touadera na Anicet Dologuele wamefanya kampeni za kurudisha usalama na kuimarisha uchumi.

Maelfu ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa na wanajeshi wa Ufaransa wanaweka usalama.