Rais mpya wa Haiti ni Jocelerme Privert

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Rais mpya wa Haiti ni Jocelerme Privert

Bunge la Haiti limemchagua rais wa mpito, juma moja baada ya aliyekuwa kiongozi wa taifa hilo Michel Martelly, kuondoka madarakani, na hivyo kuacha nchi bila ya uongozi.

Kiongozi mpya, Jocelerme Privert, alichaguliwa baada ya kikao kirefu cha bunge, ambacho kiliendelea hadi leo alfajiri.

Bwana Privert ni kiongozi wa sasa wa bunge.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Duru ya pili ya uchaguzi wa rais ilivunjwa mwezi uliopita, kwa sababu ya ghasia na tuhuma za udanganyifu.

Ataongoza nchi kwa kipindi kisichozidi miezi minne, wakati Haiti inatarajiwa kufanya uchaguzi mwengine wa rais.

Duru ya pili ya uchaguzi wa rais ilivunjwa mwezi uliopita, kwa sababu ya ghasia na tuhuma za udanganyifu.