Wapalestina 3 wauawa na Waisraeli

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Maelfu ya watu walijitokeza katika mazishi ya vijana hao

Askari wa usalama wa Israel, wamewapiga risasi na kuwauwa vijana watatu wa Palestina katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa na taifa hilo la kiyahudi.

Jeshi la Israil linasema wawili kati yao waliwashambulia kwa mawe askari waliokuwa wanapiga doria, na walitumia bastola.

Haki miliki ya picha
Image caption Askari wa usalama wa Israili, wamewapiga risasi na kuwauwa vijana watatu wa Palestina katika ufukwe wa Magharibu

Mpalestina mwengine aliuwawa baada, inavyodaiwa, kujaribu kumpiga kisu polisi wa mpakani karibu na Jerusalem na Bethlehem.

Hakuna Mu-Israili aliyeumia katika tukio hilo.