Syria: Saudia imepeleka majeshi yake Uturuki

Haki miliki ya picha AP
Image caption Syria: Saudia imepeleka majeshi yake Uturuki

Saudi Arabia imethibitisha kuwa imepeleka ndege za kijeshi katika kambi ya Uturuki, ili kuzidisha mashambulio yake dhidi ya wapiganaji wa Islamic State nchini Syria.

Kwa kupeleka ndege huko Uturuki, inamaanisha zitakuwa karibu na lengo lao Kaskazini mwa Syria.

Jenerali mmoja wa Saudi Arabia ( Ahmed al-Assiri ) alisema hakuna wanajeshi waliotumwa huko Uturuki.

Lakini aliongeza kusema, kuwa ushirika unaoongozwa na Marekani, una-o-pigana na I-S, unaamini kuwa operesheni za ardhini zitahitajika, na Saudi Arabia iko tayari kushiriki.

Image caption Kwa kupeleka ndege huko Uturuki, inamaanisha zitakuwa karibu na lengo lao Kaskazini mwa Syria

Hayo yanajiri huku rais Vladimir Putin wa Urusi na Barack Obama wa Marekani , wamekubaliana kuzidisha ushirikiano baina ya Urusi na Marekani, kuhusu Syria.

Viongozi hao waliafikiana baada ya mazungumzo kwa njia ya simu kuweka mikakati ya kumaliza vita.

Makubaliano hayo yaliafikiwa katika mazungumzo ya mjini Munich Ujerumani.

Wakizungumza kwa simu, viongozi hao wawili, pia walijadili umuhimu wa kuwa na msimamo wa pamoja dhidi ya ugaidi.

Mazungumzo kuhusu Syria yanatarajiwa kumalizika leo mjini Munich.