EU: Dunia inakabiliwa na ukweli wa vita Syria

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption EU: Dunia inakabiliwa na ukweli wa vita Syria

Na mkuu wa mashauri ya nchi za nje wa Umoja wa Ulaya,Federica Mogherini, amesema ulimwengu unakabili ukweli kuhusu Syria.

Akihojiwa na BBC, Bi Mogherini, alisema viongozi wa mataifa kadha, wanaokutana mjini Munich, sasa watekeleze makubaliano yao ya kumaliza vita:

"haya yanaweza kubadilisha hali kabisa, ikiwa ni-a hasa ni kusitisha uhasama. Huu ndio mtihani. Nia ya kisiasa ilikaririwa Alhamisi. Tumeanza kazi katika matayarisho ya kutekeleza nia hiyo. Sasa tutaona katika siku chache zijazo, iwapo nia hiyo ni ya dha-ti, na itatekelezwa. " Alisema bi Federica Mogherini

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mogherini ametaka mataifa yatekeleze makubaliano yao ya kumaliza vita nchini Syria

Katika mkutano wa usalama mjini Munich waliamua kuweka makubaliano ya ukweli kuhusu usitishaji wa vita nchini Syria katika kipindi cha wiki moja na kuanza mara moja kutolewa kwa misaada.

Amesema kuwa ulaya inafanya kila juhudi kuhakikisha kuwa mpango huo unafanikiwa ili mazungumzo ya suluhu ya kisiasa yanayoendelea kuhusu Syria yaweze kuanza mjini Geneva.