Rais wa Brazil asema Zika haitaathiri Olimpiki

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais Dilma Rousseff wa Brazil

Rais wa Brazil Dilma Rouseff amesisitiza kuwa ongezeko la visa vya virusi vya Zika halitaathiri michezo ya Olimpiki mjini Rio De Jeneiro mnamo mwezi Agosti.

Bi Rousseff amesema kuwa kukabiliana na ugonjwa huo na utafutaji wa chanjo ni swala la dharura.

Rais huyo amesema kuwa ana imani atapata ufanisi katika kuwaangamiza mbu wanaosambaza virusi hivyo.

Alijiunga na wanajeshi 2000 katika kampeni ya kitaifa ya kutoa hamasa kuhusu njia za kumaliza kuenea kwa ugonjwa huo.

Ugonjwa huo unahusishwa na kuzaliwa kwa watoto walio na kasoro.