Zahanati ya MSF yalipuliwa Idlib Syria

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mabaki ya zahanati iliyokuwa ikiendeshwa na MSF

Mashambulizi ya makombora yametekelezwa katika hospitali tatu Kaskazini mwa Syria, na kusababisha vifo vya watu kadhaa.

Shirika la kutoa misaada ya kimatibabu la MSF linasema kuwa mojawapo wa hospitali zake imeharibiwa kimaksudi katika mashambulzi ya angani katika mkoa wa Idlib.

MSF inasema kuwa takriban watu 7 wameuwawa na wanane hawajulikani waliko.

Haki miliki ya picha epa
Image caption Mashambulizi ya makombora yametekelezwa katika hospitali tatu Kaskazini mwa Syria

Hospitali nyingine katika eneo hilo pia imeshambuliwa.

Inaarifiwa kuwa hospitali hiyo imeshambuliwa kwa makombora manne katika mashambulio mawili yaliofuatana.

Kwingineko, kuna ripoti kuwa hospitali ya watoto imeshambuliwa kwa makombora katika eneo linalodhibitiwa na waasi la Azaz karibu na mpaka wa Syria na Uturuki.

Image caption MSF inasema kuwa takriban watu 7 wameuwawa

Waziri mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu ameishtumu Urusi kwa mashambulizi hayo, ambayo yamesababisha vifo vya watu 9 wakiwemo watoto.