Boko Haram ni wanafunzi wa Al shabab

Haki miliki ya picha Boko Haram video
Image caption Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud amesema kuwa anaushahidi wa kutosha kuwa wapiganaji hao wa Boko Haram walijifunzia ugaidi nchini humo.

Wapiganaji wa kiislamu wa Boko Haram wanaosababisha maafa mengi nchini Nigeria walijifunza ukatili wao kutoka kwa al Shabab nchini Somalia.

Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud amesema kuwa anaushahidi wa kutosha kuwa wapiganaji hao wa Boko Haram walijifunzia ugaidi nchini humo.

''Magaidi wanauhusiano na kila mara wanasaidiana kubadilishana mbinu na mawazo ya kuetekeleza maafa zaidi'' alisema rais Mohamud.

''Jamii ya kimataifa haina budi ila kuisaidia Somalia kupamabana dhidi ya Al Shabaab'' aliongezea rais huyo.

''Bila shaka tunaushahidi mkubwa kuwa Boko Haram ni wanafunzi wa Al Shabab''

Haki miliki ya picha AP
Image caption ''tunaushahidi mkubwa kuwa Boko Haram ni wanafunzi wa Al Shabab'' rais Mohamud

''Iwapo Somalia itapata amani Afrika bila shaka itakuwa na amani'' aliongezea rais huyo.

Rais Hassan Sheikh Mohamud aliyasema hayo alipokuwa akihutubia mkutano wa usalama wa kimataifa uliokamilika mjini Munich Ujerumani siku ya Jumapili.