UN yatafuta amani ya Syria

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Syria Walid al Moallem

Kikosi maalumu cha umoja wa mataifa kikiongozwa na , Steffan de Mistura, kimewasili salama katika mji mkuu wa Damascus nchini Syria kwa lengo la kujaribu kusaidia kufikia hatua ya kusitisha mapigano.

Maofisa wa serikali nchini Syria wamesema kwamba bwana Mistura alifanya mazungumzo na waziri wa mambo ya nchi za nje wa nchi hiyo Walid al-Moallem mapema wiki hii, na kusema kwamba mazungumzo hayo yanafuatia mazunguzo ya awali yaliyofanyika mjini Munic , mkutano ambao viongozi wenye ushawishi mkubwa walikubaliana kukomesha uhasama baina ya pande hasimu ili kuruhusu misaada ya kibinaadamu kuingia nchni Syria .