Al-Shabab wavamia kambi ya jeshi Somalia

Image caption Wapiganaji wa al-shabab

Wapiganaji wa kundi la kigaidi la al-Shabab wamevamia vituo vya polisi pamoja na kambi ya wanajeshi karibu na mji mkuu wa Somalia Mogadishu.

Mji wa Afgoye ulionekana kuwa eneo salama, japo wapiganaji hao walivamia nyakati za usiku na kuua watu kumi, wengi wao wakiwa wanajeshi wa asili ya kisomali.

Wapiganaji hao wa al Shabab walichukua silaha kali na magari ya kijeshi.

Wanajeshi wa Umoja wa Afrika wanasaidi wanajeshi wa Somalia kulinda taifa hilo, japo mashambulizi ya hivi karibuni yamedhoofisha usalama nchini humo.