Ambwene Yesaya a.k.a AY
Huwezi kusikiliza tena

AY awatakia Waganda kila la kheri

Zimesalia Saa ishirini na nne kutoka sasa wananchi wa Uganda wataelekea kwenye sanduku la kupigia kura, ili kumpa ridhaa kiongozi wamtakaye ili awaongoze.

Ulimwengu na waangalizi wa kimataifa wameelekeza macho na masikio nchini Uganda kufuatilia yanayojiri kuanzia kampeni,uchaguzi na hatimaye matokeo ya kutangazwa kwa mshindi wa uchaguzi ho katika nafasi ya uraisi na kwa upande mwingine wabunge na madiwani pia watachaguliwa.

Kutokana na hali hiyo basi ukanda wa maziwa makuu si wanasiasa tu wanaofuatilia uchaguzi huo bali kwa namna ya pekee mwanamuziki wa miondoko ya HIP HOP ama kwa maelezo yake ni nguli wa muziki wa kibiashara zaidi kutoka nchini Tanzania, namzungumzia Ambwene Yesaya analo la kusema juu ya uchaguzi wa Uganda, alipokutana na mwandishi wetu Arnold Kayanda, Ambwene ana tiririka namna hii…….