Shambulio la hospitali ni uhalifu wa kivita

Haki miliki ya picha
Image caption Hospitali ya Syria ilioshambuliwa

Ufaransa na Uturuki zimesema kuwa mashambulio ya angani yaliolenga hospitali Kaskazini mwa Syria yanashirikisha uhalifu wa kivita.

Hadi watu 50 wameuawa katika mashambulio katika hospitali na shule katika jimbo hilo,kulingana na umoja wa Mataifa.

Wizara ya maswala ya kigeni nchini Uturuki imelaumu Urusi kwa shambulio hilo.Moscow hatahivyo haijatoa tamko lake kuhusu madai hayo.

Haki miliki ya picha epa
Image caption hospitali

Wakati huohuo rais wa Syria Bashar al Assad ana wasiwasi kuhusu mpango wa kusitisha vita nchini Syria.

Wiki iliopita mataifa yenye uwezo mkubwa duniani yalikubaliana kushirikiana kupitia makubaliano ya amani ,ambayo yataanza baadaye wiki hii.

Lakini katika matamshi yake kuhusu tangazo hilo,Rais Assad alisema kuwa usitishwaji huo wa vita haumaanishi kwamba pande zote zitaweka chini silaha zao.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption mashambulio ya Syria

''Kwa sasa wanasema kuwa wanataka vita visitishwe kwa juma moja'',alisema katika runinga.''Ni nani anayeweza kufuatilia masharti haya yote na mahitaji yake kwa juma moja''?.

Umoja wa Mataifa unasema kuwa misururu ya mashambulizi kaskazini mwa Syria inatilia shaka kuhusu masharti hayo ya kusitisha vita.