Virusi vya Zika vyapatikana katika ubongo

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mama aliye na mtoto mwenye virusi vya Zika

Ushahidi zaidi unaohusisha virusi vya Zika na kasoro ya maumbile miongoni mwa watoto umepatikana,wanasayansi nchini Brazil Wamesema.

Wasayansi hao kutoka chuo kikuu cha PUC-Parana University wamegundua virusi hivyo ndani ya ubongo wa watoto wawili ambao waliishi kwa saa 48 pekee.

Image caption Zika

Virusi hivyo vinavyosababishwa na mbu vinasababisha kasoro ya watoto kuwa na vichwa vidogo mbali na ubongo ulioharibika.

Brazil ina takriban visa 460 vya ugonjwa huo na inachunguza visa vingine 3,850.Virusi hivyo vimesambaa katika eneo la Marekani kusini,lakini Brazil imeathiriwa zaidi.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Zika

Wanasayansi wameiambia BBC kwamba violezi vilivyochukuliwa kutoka kwa ubongo wa watoto hao vilionyesha kuwa virusi hivyo vya Zika vilikuwa hai ndani ya ubongo.

Wanasayansi hao wamekuwa wakifuatilia mimba za wanawake 10 wajawazito katika jimbo la Kaskazini mashariki mwa Paraiba,ambalo ni la pili kwa visa vya ugonjwa huo.