Apple yapinga amri ya kuifungua simu ya muuaji

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mkurugenzi mkuu wa Apple Tim Cook

Apple itapinga amri ya mahakama ya kuwasaidia wachunguzi wa shirika la kijasusi nchini Marekani FBI kuchukua habari katika simu ya muuaji wa watu 14 katika eneo la San Bernadinho nchini Marekani.

Kampuni hiyo ilikuwa imeamrishwa kulisaidia shirika hilo la FBI kuifungua simu ya aina ya iphone ya Farook Syed ambayo wanasema ina habari muhimu.

Katika taarifa ,mkurugenzi mkuu wa Apple Tim Cook amesema:Serikali ya Marekani inaitaka Apple Kuchukua hatua kama hizo ambazo zinatishia usalama wa wateja wetu.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Farook na mkewe

Tunapinga amri hiyo ambayo ina athari zaidi ya kesi iliopo.

Tangu kutolewa kwa programu mnamo mwezi Septemba 2014,data ya simu za Apple kama vile ujumbe na picha zimewekewa usalama wa kutosha.

Hii ina maanisha kwamba iwapo simu hiyo imefungwa ,ni nywila au neno la siri la simu hiyo linaloweza kuifungua na kupata data hiyo.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kampuni ya Apple

Iwapo mtu atajaribu mara 10 bila mafanikio data iliopo ndani ya simu hiyo hujifuta .

Hakuna mtu ama hata kampuni ya Apple itaweza kupata ujumbe huo,hatua ambayo kampuni hiyo ilifanya kufuatia ufichuzi wa bwana Edward Snowden kwamba serikali ya Marekani imekuwa ikidukua simu za raia.