Kambi ya Boko Haram yaharibiwa Nigeria

Image caption Kambi ya Boko Haram

Jeshi la Nigeria limesema kuwa limeharibu kambi za wapiganaji wa Boko Haram katika vijiji vya Doro na Kuda kaskazini mashariki mwa jimbo la Borno.

Wapiganaji wanne wa kundi hilo waliuawa huku wengine wawili wakikamatwa wakati wa oparesheni katika misitu ya eneo la Alagarno na Sambisa,kulingana na msemaji wa jeshi kanali sani Usman.

Wanajeshi watatu na raia wanne walijeruhiwa katika mapigano hayo, alisema.

Haki miliki ya picha Nigeria Army
Image caption Jeshi la NIgeria

Pikipiki,farasi na Punda walipatikana katika kambi hiyo.

Kundi la Boko haram limepoteza eneo kubwa lililokuwa likidhibiti, lakini bado linatekeleza milipuko mibaya ya kujitolea muhanga.