Viwango vya kutisha vya sukari katika vinywaji

Image caption Vinywaji vya moto vilivyo na viwango vya juu vya sukari

Kuna viwango vya sukari ya juu vinavyoshangaza katika vinywaji vya moto vinavyouzwa katika migahawa,kundi moja limeonya.

Kundi hilo limesema kuwa kuna vinywaji 131 vilivyokolea sukari huku likifichua kwamba thuluthi moja ya vinjwaji hivyo vina sukari zaidi ya Soda za Pepsi na Coca- Cola ambazo zina vijiko tisa vya sukari.

Shirika hilo la hisani limesema kuwa katika visa vibaya zaidi,vinywaji hivyo vina zaidi ya vijiko ishirini vya sukari.

Migahawa ya kuuza chai kama vile Starbucks,Costa na Caffe Nero vimesema kuwa viko tayari kupunguza sukari katika vinywaji vyao.

Professa Graham Mac Gregor ,ambaye ni mwenyekiti wa vita dhidi ya Sukari amesema ni mfano mwengine wa kashfa ya viwango vya sukari katika vyakula vyetu na vinywaji.''Ndio maana tuna viwango vya juu vya ugonjwa wa kunenepa kupitia kiasi barani Ulaya'',alisema.

Image caption Viwango vya sukari

Vinywaji vilivyochunguzwa ni pamoja na kahawa kama vile Mochas na Lattes,vinywaji vya matunda,vile vya chokoleti kutoka kwa maduka ya kahawa na maduka ya kuuza vya kula vya milolongo.

Shirika hilo lilibaini kwamba asilimia 98 ya vinywaji vilivyopimwa vitaorodheshwa kama vinywaji vyenye sukari nyingi .

Kiwango cha sukari kinachohitajika kwa siku miongoni mwa watu walio juu ya umri wa miaka 11 ni gramu 30 au vijiko sita,huduma ya kitaifa ya afya imesema nchini Uingereza.