Mambo muhimu kuhusu uchaguzi wa Uganda

wagombea
Image caption Kuna wagombea wanane wa urais katika uchaguzi wa sasa

Uchaguzi mkuu nchini Uganda unafanyika leo, wengi wakiangazia sana uchaguzi wa urais ambapo kuna jumla ya wagombea wanane.

Mwanamke ni mmoja, Maureen Kyalya.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahidi kwamba matokeo yatakuwa tayari katika kipindi cha saa 48 baada ya kufungwa kwa vituo saa kumi alasiri.

Baada ya hapo, tume inatarajia kuwa ikitangaza matokeo ya urais baada ya kila saa mbili.

Mwenyekiti wa tume Badru Kiggundu aliambia wanahabari Jumatano kwamba huenda wakakosa kutoa matokeo mwendo wa saa thenashara leo lakini baada ya hapo watawapasha watu kuhusu matokeo kila baada ya saa mbili kupita.

Kituo cha taifa cha kuhesabia na kutangazia matokeo kinapatikana katika uwanja wa Mandela, Namboole eneo la Bweyogerere wilayani Wakiso.

Ili kutangazwa mshindi, mgombea anafaa kupata asilimia 50 ya kura zilizopigwa na kura moja juu. Hili likikosa kufanyika, kunafaa kuwa na duru ya pili ya uchaguzi ikishirikisha wagombea wawili waliopata kura nyingi zaidi.

1. Wagombea urais ni kina nani?

Ndio hawa hapa:

 • Abed Bwanika – Peoples Development Party
 • Amama Mbabazi – Go Forward
 • Benon Biraaro - Mgombea huru
 • Joseph Mabirizi- Mgombea huru
 • Kizza Besigye – Forum for Democratic Change
 • Maureen Kyalya – Mgombea huru
 • Venansius Baryamureeba - Mgombea huru
 • Yoweri Museveni – National Resistance Movement

2. Wapiga kura ni wangapi?

Kuna wapiga kura 15,277,196 waliosajiliwa nchini Uganda, na vituo 28,010 vya kupigia kura.

3. Maeneo Bunge ni mangapi Uganda?

Kuna maeneo bunge 290 nchini Uganda.

4. Uchaguzi mkuu wa 2011 na 2006 matokeo ya uchaguzi wa rais yalikuwaje?

Matokeo ya uchaguzi 2011
 • Yoweri Kaguta Museveni (NRM): 68.38%
 • Besigye Kizza (FDC): 26.01%
 • Mao Norbert (DP): 1.86%
 • Abed Bwanika (PDP): 0.65%
 • Olara Otunnu (UPC) 1.58%
 • Beti Olive Kamya Namisango (UFA): 0.66%
 • Bidandi-Ssali Jaberi (PPP): 0.44%
 • Samuel Lubega Mukaaku Walter (mgombea huru): 0.41%
Matokeo ya uchaguzi wa 2006
 • Yoweri Kaguta Museveni (NRM): 59.26%
 • Besigye Kizza (FDC): 37.39%
 • Ssebaana J. Kizito (DP): 1.58%
 • Abed Bwanika (Mgombea huru): 0.95%
 • Obote Kalule Miria (UPC) 0.82%

5. Kuna vyama vingapi vya siasa Uganda?

Kuna vyama na mashirika ya siasa 29 nchini Uganda ambayo yamesajiliwa.

 1. Activist Party (AP)
 2. Congress Service Volunteers Organisation (COSEVO)
 3. Conservative Party (CP)
 4. Democratic Party (DP)
 5. Ecological Party of Uganda (EPU)
 6. Farmers Party of Uganda (FPU)
 7. Forum for Democratic Change (FDC)
 8. Forum for Integrity in Leadership (FIL)
 9. Green Partisan Party (GPP)
 10. Justice Forum (JEEMA)
 11. Liberal Democratic Transparency (LDT)
 12. National Convention For Democracy (NCD)
 13. National Peasants’ Party (NPP)
 14. National Resistance Movement (NRM)
 15. National Unity, Reconciliation and Development Party (NURP)
 16. National Youth Revolutionary Organisation (NYRO)
 17. Social Democratic Party(SDP)
 18. People’s Development Party (PDP)
 19. People’s Progressive Party (PPP)
 20. Popular People’s Democracy (PPD)
 21. People’s United Movement (PUM)
 22. Republican Women and Youth Party (RWYP)
 23. Revolutionary People’s Party (RPP)
 24. Society for Peace and Development (SPD)
 25. Uganda Economic Party (UEP)
 26. Uganda Federal Alliance (UFA)
 27. Uganda Patriotic Movement (UPM)
 28. Uganda People’s Congress (UPC)
 29. Uganda People’s Party (UPP)
Image caption Amama Mbabazi anatumia chama cha Go Forward