Makundi hasimu yapigana Sudan Kusini

Image caption Majeruhi

Sudan Kusini imeshuhudia mapigano makali yaliyodumu usiku kucha katika kambi ya watu wasio na makaazi kwenye mji wa Malakal huko Sudan Kusini.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa ulioko nchini humo wamearifu kuwa watu watano wamepoteza maisha na wengine wapatao thelathini kujeruhiwa vibaya.

Kambi hiyo imo ndani ya wigo wa Umoja wa mataifa ni mahali ambako wanahifadhiwa karibu watu elfu hamsini ambao hawana makazi baada ya kusambaratishwa na vita.

ujumbe huo wa umoja wa mataifa umearifu kwamba mapigano hayo yalikuwa ni baina ya makundi mawili ya vijana hasimu ya kikabila ya Shilluk na Dinka .

Haki miliki ya picha Reuters

Mji wa Malakal umeingia katika mabadiliko ya kila namna tangu kipindi cha mgogoro ulioanza mwishoni mwa mwaka 2013 wakati huo rais Salva Kiir akishutumiana na makamu rais wake Riek Machar kwa kupanga njama za mapinduzi.