Mwandishi wa To Kill A Mockingbird afariki dunia

Harper Lee, mwandishi wa kitabu mashuhuri duniani cha To Kill A Mockingbird, amefariki akiwa na umri wa miaka 89.

Habari za kifo chake zimethibitishwa na meya wa mji alimokuwa akiishi wa Monroeville, Alabama.

Alizaliwa na kupewa jina Nelle Harper Lee 28 Aprili 1926.

Mwaka 1960, alichapisha kitabu How To Kill A Mockingbird, ambacho kilifanikiwa sana na kumsaidia kushinda tuzo ya fasihi Pulitzer katika ubunifu.

Kitabu hicho kiliuza nakala 30 milioni kote duniani.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Harper Lee alikuwa na umri wa miaka 89

Hakutoa kitabu kingine hadi mwaka uliopita, kitabu kwa jina Go Set A Watchman kilipochapishwa.

Alikuwa kitindamimba wa mwanasheria Amasa Coleman Lee na Frances Cunningham Finch Lee.

Alikuwa mtu mnyamavu na mpenda usiri sana na aliheshimiwa sana na wakazi wa mji alimoishi.

Haki miliki ya picha

Ilikuwa nadra sana kwake kukubali kuhojiwa na wanahabari.