Pacquiao awakosoa tena wapenzi wa jinsia moja

Haki miliki ya picha AP
Image caption Pacquio

Bondia wa Filipino na mwanasiasa Manny Pacquiao amerejelea msimamo wake wa wapenzi wa jinsia moja ,baada ya kuomba msamaha hapo awali akisema ''ni wabaya zaidi ya wanyama''.

''Kile ninachosema ni ukweli .Nazungumza ukweli,kile bibilia inachosema,''alisema katika eneo la mazoezi nyumbani kwake huko General Santos.

Bondia huyo amesema makosa yake makubwa ni kumfananisha mwanadamu na mnyama.

Kampuni ya Nike ilifutilia mbali mkataba wake ,na bondia huyo ikiyataja matamshi yake kuwa ''ya adui''.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Jason Collins

Matamshi yake yalishtumiwa duniani kote akiwemo mchezaji wa mpira wa kikapu Jason Collins ambaye ni mpenzi wa jinsia mmoja pamoja na Floyd Mayweather aliyemshinda katika pigano lake la mwezi Mei.

Bwana Pacquiao baadaye aliomba msamaha katika mtandao wake wa facebook,akisema kuwa amewakosea binadamu na kwamba hakuushtumu muungano wa wapenzi wa jinsia moja,bali hakuwa anaunga mkono ndoa za jinsia moja.