Al-Qaida wateka mji wa Ahwar, Yemen

Haki miliki ya picha AFP Getty
Image caption Yemen

Inaarifiwa kuwa wapiganaji kadha wa al-Qaeda nchini Yemen, wameuteka mji wa Ahwar, Kusini mwa Yemen.

Duru za huko zinanukuliwa kusema kwamba, wakati wapiganaji walipoingia mjini humo, walipambana na kikosi kilichokuwa kikilinda mji huo na watatu waliuwawa.

Vilevile wapiganaji waliweka vizuizi vya barabarani na kupandisha bendera yao katika majengo ya serikali.

Wadadisi wanasema, kwa kuteka mji wa Ahwar, itaisaidia al-Qaeda kujizatiti katika mwambao wa jimbo la Abyan, ambako tayari inadhibiti miji mengine miwili.