Hull City yaizuia Arsenal katika FA

Haki miliki ya picha All Sport
Image caption Arsenal dhidi ya Hull City

Mabingwa watetezi wa kombe la FA Arsenal ni lazima waende Hull City kwa mchuano wa marudiano wa raundi ya tano baada ya kushindwa kuimarisha utawala wao ili kushinda mechi hiyo.

The Gunners walidai kunyimwa penalti mbili na walikuwa na nafasi chungu nzima kushinda mechi hiyo kupitia washambuliaji Walcott na Wellbeck.

Kipa wa Hull City Eldin Jakupovic alilazimika kufanya kazi ya ziada na kuokoa mashambulio mengi,hususan krosi ya Joel Campbell iliopiga chuma cha goli lake.

Hull City ilitengeza nafasi chache lakini walililinda lango lao .

Timu hizo mbili zilifanya mabadiliko 19 kati yao mongoni mwa wachezaji ikilinganishwa na mechi zao walizocheza hapo awali.