California yakataa kondomu katika filamu za ngono

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mipira ya kondomu

Maafisa wa usalama kazini katika jimbo la California nchini Marekani wamepiga kura ya kutowalazmisha nyota wa filamu za ngono kuvaa mipira ya kondomu ili kuzuia kuenea kwa magonjwa ya zinaa.

Wawakilisha wa filamu hizo walihoji kwamba mipira ya kondomu huenda isiwavutie wateja wao na hivyobasi kuharibu soko la filamu hizo.

Wameonya kwamba uamuzi wa kuwalazimisha nyota hao kuvaa mipira ya kondomu huenda ukawalazimu nyota wa filamu hizo kuvaa miwani ya kuhifadhi macho pamoja na vifaa vya kuzuia meno.

Wanaoshiriki katika filamu hizo hulazimika kupimwa magonjwa ya zinaa kila baada ya majuma mawili.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wakaazi wa California wakifamnya maandamano ya kushinikza nyota wa filamu za ngono kuvaa mipira ya kodomu

Kura hiyo inajiri baada ya Hazina ya afya ya ugonjwa wa ukimwi kutaka idara ya maafisa wa usalama kazini mjini California kuweka sheria kali za kiafya katika viwanda vinavyozalisha filamu za ngono.

Lakini wawakilishi wa filamu hizo wamesema kuwa iwapo nyota wa filaumu hizo watalazimishwa kuvaa mipira ya kondomu huenda ikaathiri soko la filamu hizo.