Kylie Minogue achumbiwa

Image caption Kylie Minogue

Mwanamuziki Kylie Minogue ametangaza kuwa yeye ni mchumba wa Joshua Sasse.

Baada ya wiki kadhaa za uvumi,wawili hao wametoa tangazo rasmi kwa kuweka notisi katika gazeti la Daily Telegraph nchini Uingereza.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 47 amekuwa akionekana na nyota huyo wa filamu nchini Uingereza kwa kipindi cha miezi sita.

Inadaiwa huenda nyota huyo wa filamu alianzisha mjadala huo wa kutaka kumchumbia Monogue wakati wa Christmas.

Siku chache zilizopita katika tuzo ya NME ,Kylie alionekana amevalia kipande kikubwa cha pete ya almasi.

Wawili hao walikutana mwaka uliopita,wakati Joshua alipokuwa akicheza filamu ya ucheshi ya Gallavant.