Takriban watu 140 wauawa Syria

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mji wa Homs ni Mji ulioshuhudiwa machafuko makubwa zaidi

Takriban watu 140 wameuawa kwa milipuko ya mabomu katika miji ya Homs na Damascus nchini Syria, waangalizi na vyombo vya habari vya serikali vimeeleza.

Takriban milipuko minne ilitokea katika eneo la Sayyida Zeinab mjini Damascus na kuua takriban watu 83. Awali mjini Homs Watu 57 wengi wao raia waliuawa kwa mashambulizi ya mabomu yaliyokuwa yametegwa kwenye magari mawili.

Wanamgambo wa Islamic State wamekiri kutekeleza mashambulizi hayo katika miji hiyo miwili.

Wakati huo huo, Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani, John Kerry amesema makubaliano ya muda yamefikiwa kati Marekani na Urusi kuhusu suluhu ya mgogoro wa Syria.