Hillary Clinton ameshinda jimbo la Nevada

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Bi Hillary Clinton ameshinda kura za mchujo za jimbo la Nevada

Muaniaji bendera ya urais wa chama cha Democratic nchini Marekani Bi Hillary Clinton ameshinda kura za mchujo za jimbo la Nevada.

Bi Clinton, alibwaga mpinzani wake Bernie Sanders, kwa asilimia tano katika mchujo wa huko Nevada.

Bi Clinton aliwashukuru wafuasi wake waliomshangilia kwa shangwe vifijo na nderemo huku akisema kuwa hajawahi kuwa na shaka kuhusu matokeo hayo.

Sanders ambaye umaarufu wake ameimarika katika siku za hivi punde alisema kuwa japo wameshindwa walifaulu kupunguza pengo kati yake na Hillary Clinton aliyepigiwa upatu kutwaa tikiti ya chama cha Democrats