India: 10 wauawa, ukosefu wa maji New Delhi

Haki miliki ya picha Anoop Thakur
Image caption 10 wauawa kufuatia ukosefu wa maji India

Watu 10 wameuawa India kufuatia siku tatu za machafuko kupinga sera za ubaguzi wa matabaka na utoaji wa maji kwa mgao.

Ghasia hizo zilianzishwa na watetezi wa haki za matabaka mbalimbali hasa katika jimbo la Haryana.

Watu wa tabaka la Jat walizua kihoja wakilalamikia kubaguliwa katika utoaji nafasi za ajira na hata elimu.

Image caption Walikabiliana na polisi wa kupambana na ghasia pamoja na kikosi cha jeshi la taifa.

Walikabiliana na polisi wa kupambana na ghasia pamoja na kikosi cha jeshi la taifa.

Waandamanaji hao waliharibu rasilimali kubwa katika eneo la bwawa kubwa la Munak, chanzo cha maji yanayotumika mjini New Delhi .

Maafisa wa serikali ya mji wa Delhi, wameanzisha shughuli za kutoa maji kwa mgao.

Image caption Wanadai kutengwa kwa kuwanyima elimu na nafasi za kazi serikalini.

Wanaonya kuwa kuna baadhi ya maeneo katika mji huo ambayo yatakosa maji kuanzia leo Jumapili.

Shule zote zitafungwa kuanzia kesho Jumatatu.

Waandamanaji hao wa jamii ya Jat wana hasira kuhusiana na sheria za India za kuwabagua watu kitabaka.

Haki miliki ya picha PTI
Image caption Wanadai kutengwa kwa kuwanyima elimu na nafasi za kazi serikalini.

Mji mkuu wa India, New Delhi unakabiliwa na uhaba mkubwa wa maji kufuatia ghasia hizo.

Waandamanaji hao wa tabaka hilo la Jat wanataka serikali iwape mgao wa nafasi za kazi sawa na watu wa matabaka ya chini.

Hata hivyo wachanganuzi wanadai kuwa Jat hawastahili kujumishwa katika matabaka maskini kwani wanauwezo mkubwa na pia wanatumia idadi yao kubwa kuishinikiza serikali.

Waandamanaji wamekiuka amri ya kutotoka nje na hata wametishia kusimamisha usafiri wa reli ambayo ni nguzo muhimu ya uchukuzi nchini India.