Watu 6 wapigwa risasi na kuuawa Marekani

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Watu sita wauawa kwa kupigwa risasi Marekani

Watu sita wauawa kwa kupigwa risasi MarekaniPolisi wanamzuilia mwanamume mmoja eneo la Kalamazoo, jimbo la Michigan, Marekani baada ya watu sita kuuawa kwa kupigwa risasi na mtu asiyejulikana.

Watu wanne waliuawa katika mgahawa mmoja na wengine wawili katika duka la kuuza magari.

Maafisa wanasema mwanamume aliyetekeleza mauaji hayo alikuwa zunguka eneo hilo akiwafyatulia risasi watu kiholela.

Mashambulio hayo yanadaiwa kuwa na uhusiano na kisa cha awali cha ufyatuaji wa risasi katika maegesho ya magari, ambapo mwanamke mmoja alijeruhiwa vibaya.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Watu wanne waliuawa katika mgahawa mmoja na wengine wawili katika duka la kuuza magari.

Polisi wa Kalamazoo wamethibitisha kwamba wanamzuilia mwanamume huyo lakini wakasema bado wanaendelea na uchunguzi.

"Hivi ni visa vya kusikitisha sana na tunaendelea na uchunguzi kubaini iwapo tumemkamata mshukiwa aliyetekeleza mauaji,” polisi hao wameandika kwenye ukurasa wao wa Facebook.

“Haya ni mauaji ya kutekelezwa kiholela,” mkuu wa polisi wa Kalamazoo Paul Matyas amesema.