46 wauawa Syria huku Marekani na Urusi zikikutana

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wanaharakati nchini Syria wanasema kuwa watu kama 46 wameuawa, kwenye milipuko sambamba ya mabomu

Wanaharakati nchini Syria wanasema kuwa watu kama 46 wameuawa, kwenye milipuko sambamba ya mabomu, katika mji wa Homs, Magharibi mwa nchi.

Shirika la haki za kibinaadamu la Syria, lenye makao yake Uingereza, (Syrian Observatory for Human Rights) linasema kuwa dalili zinaonesha wengi waliouwawa, walikuwa ni raia.

Shirika hilo linasema milipuko yote miwili, ilitokana na mabomu yaliyotegwa kwenye magari, yaliyolipuka katika mtaa wenye wafuasi wengi wa Rais Bashar al-Assad.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Haijulikani nani alitekeleza mashambulizi hayo

Haijulikani nani alitekeleza mashambulizi hayo, lakini eneo hilo limewahi kulengwa namna hiyo, na wapiganaji wa Islamic State.

Na akizungumza na waandishi wa habari mjini Amman, akiwa kando ya mwenzake wa Jordan, waziri wa mashauri ya nchi za nje wa Marekani, John Kerry, alisema, anatumai kuwa makubaliano ya kusitisha mapigano nchini Syria, yanaweza kufikiwa haraka.

Bwana Kerry alisema kuwa, amezungumza na mwenzake wa Urusi, Sergei Lavrov, saa moja kabla...

Haki miliki ya picha AFP
Image caption John Kerry, alisema, anatumai kuwa makubaliano ya kusitisha mapigano nchini Syria, yanaweza kufikiwa haraka

"Naamini kuwa katika mazungumzo yetu, tumefikia makubaliano ya kimsingi, kuhusu usitishwaji wa mapigano, ambayo yanaweza kuanza kutekelezwa katika siku zijazo. Bado hayakukamilika.''

''Hata hivyo natumai kuwa marais wetu, Obama na Putin, huenda wakazungumza katika siku chache zijazo, ili kujaribu kumaliza kazi hii." alisema Bwana Kerry.