Watu milioni 10 hawana maji New Delhi

Haki miliki ya picha AP
Image caption Jeshi nchini India limetwaa udhibiti wa mfereji ambao unapeleka maji katika mji mkuu wa New Delhi.

Zaidi ya watu milioni 10 wakaazi wa mji mkuu wa India New Delhi waliamka leo na kupata mifereji yao imekauka.

Mkurugenzi mkuu wa kampuni inayotoa huduma ya maji mjini humo bwana Keshav Chandra amesema kuwa itawachukua takriban siku nne kurejesha hali ya kawaida na maji kote mjini humo.

Haki miliki ya picha Delhi Jal Board
Image caption Bomba la maji la Munak lililoharibiwa na watu wa tabaka la Jat

Chandra aliyasema hayo hata baada ya serikali kusema kuwa jeshi nchini India limetwaa udhibiti wa mfereji ambao unapeleka maji katika mji mkuu wa New Delhi.

Mfereji huo ulioharibiwa wakati wa ghasia za siku kadhaa iliyosababishwa na waandamanaj wa tabaka la Jat.

Image caption Watu 16 wameuwa na mamia ya wengine kujeruhiwa.

Udhibiti wa bomba hilo la Munak ambalo linaripotiwa kupeleka asilimia 60% ya maji yanayotumiwa mjini Delhi utasaidia kurejesha huduma hiyo muhimu.

Huduma hizo za maji zilikatwa wakati wa siku tatu za maandamano mabaya katika jimbo lililo karibu la Haryana kutoka kwa watu wanaolalamikia ajira na ufadhili wao na serikali.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Huduma hizo za maji zilikatwa wakati wa siku tatu za maandamano mabaya katika jimbo lililo karibu la Haryana

Watu 16 wameuwa na mamia ya wengine kujeruhiwa.

Shule zote za mji wa Delhi zimefungwa kutokana na tatizo la uhaba wa maji.