Mpango wa kusitisha vita kuanza Syria

Haki miliki ya picha AP
Image caption Maelfu ya Watu wamepoteza maisha kutokana na mapigano nchini Syria

Marekani na Urusi zimetangaza mpango wa kusitisha mapigano nchini Syria kuanza kutekelezwa saa sita usiku wa tarehe 27 mwezi Februari.

Kauli yao imesema makubaliano hayo hayajahusisha kundi la wanamgambo wa Islamic State na wanamgambo wanaungwa mkono na Al Qaeda Nusra Front.

Mataifa yenye nguvu duniani yalikubaliana tarehe 12 Februari kuwa utekelezaji wa makubaliano hayo ufanyike ndani ya wiki moja, lakini muda huo ulipita na hivi sasa wanatazama mipango mipya.

Siku ya jumapili Watu 140 waliuawa kutokana na mashambulizi ya mabomu mjini Homs na Damascus.

Zaidi ya raia 250,000 wameuawa kutokana na mgogoro wa nchini humo ulioanza mwezi March mwaka 2011.

Takriban watu milioni 11 wameyakimbia makazi yao huku wengine milioni nne waliitoroka Syria na kufanya kufanya safari zilizoathiri maisha yao wakielekea barani Ulaya.