Ban Ki-moon: Nkurunziza kuzungumza na upinzani

Haki miliki ya picha
Image caption Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi amekubali kufanya mazungumzo na upinzani.

Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi amekubali kufanya mazungumzo na upinzani.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa bwana Ban Ki-moon amesema kuwa rais Nkurunziza ameitikia mwito wa mazungumzo ya upatanishi yanayolenga kumaliza miezi 10 ya mzozo wa kisiasa.

Ban ambaye yuko mjini Bujumbura katika ziara maalum amesema kuwa rais huyo pia amekubali kuwaachilia huru wafungwa 2000.

mamia ya watu wameuawa katika makabiliano baina ya vyombo vya dola na wafuasi wa upinzani.

makabiliano yalianza mwezi Aprili mwaka uliopita rais Nkurunziza alipotangaza nia ya kuwania awamu ya 3 ya urais katika uchaguzi mkuu.

Wapinzani wake walidai kuwa rais huyo alikuwa anakiuka katiba ya nchi inayomtaka kiongozi asitawale kwa zaidi ya vipindi viwili.

Nkurunziza naye anashikilia kuwa hakuchaguliwa wakati wa awamu ya kwanza ya utawala wake uliofuatia mazungumzo ya kusitisha mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.

Zaidi ya watu lakini mbili u nusu wametorokea mataifa jirani.