Mars yataka Chokoleti zirudi kiwandani

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Nchi hamsini na tano zatakiwa kurejesha Chokoleti kiwandani

Watengenezaji wa chokoleti za Mars nchini Marekani wamesema inazitaka nchi hamsini na tano kurejesha mamilioni ya chokoleti, madai hayo yamekuja baada ya mteja mmoja kutoka Ujerumani kukuta vipande vya plastiki katika moja ya bidhaa hiyo.

Wanasema bidhaa ambayo wanaizungumzia imetengenezwa Uholanzi na boksi lake lilichanganya vipande vya chokoleti vya Mars, Snickers na Milky Way.

Katika kuhakikisha kuwa bidhaa zao zote zina ubora,Kampuni ya Mars inataka kujiridhisha kwa kuzirejesha chokoleti zote za kampuni yao zilizopo sokoni kurudi kiwandani.

Mars imesema kuwa tarehe za matumizi bora ya bidhaa yao ilikuwa kati ya Juni mwaka huu na Januari mwaka ujao.

Hata hivyo kampuni hiyo haijasema ni chokoleti ngapi zimeathirika au zitawagharimu hasara ya kiasi gani?

Bali Mars imetoa taarifa ya kuomba radhi wateja wake.