Mgombea wa urais amfuta kazi msemaji wake US

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Ted Cruz

Mgombea wa urais nchini Marekani Ted Cruz amemtaka msemaji wa kampeni yake kujiuzulu baada ya afisa huyo kukuza kanda ya video iliokarabatiwa ya mpizani wake Marco Rubio.

Rick Tyler alichapisha katika mtandao wake wa Tweeter habari na video iliomuonyesha bwana Rubio akikitaja kitabu cha Bibilia ''kama kitabu kizuri kisichokuwa na majibu ndani yake''.

Kampeni ya bwana Rubio ilisema:''Majibu yote yako ndani''.

Hatua hiyo inajiri baada ya kampeni ya bwana Cruz kudaiwa kuwa na hila za uwongo na uchafu na kampeni za wapinzani wake.

''Kampeni yetu isingeituma,''bwana Cruz aliwaambia maripota siku ya jumatatu.Kampeni yetu haiwezi kuuliza maswali mengi kuhusu ''imani ya mgombea mwengine''.

Bwana Tyler,ambaye ni mkurugenzi wa mawasiliano aliomba msamaha kwa kampeni ya Rubio katika chapisho la facebook.