Binti mfalme akiwacha choo kilichogharimu $40,000

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Choo cha binti mfalme wa Cambodia

Choo kilichogharimu dola 40,000 cha binti mfalme wa Thailand aliyezuru nchini Cambodia kiliwachwa bila kutumiwa ,maafisa wanasema.

Binti Mfalme Maha Chakri Sirindhorn aliripotiwa kupiga picha jengo la choo hicho wakati wa ziara yake ya eneo la Yeak Lom Lake ,Kaskazini mashariki mwa Cambodia.

Choo hicho sasa kimeondolewa na jengo hilo limebadilishwa na kuwa afisi ya utalii.

Image caption Jengo la choo hicho sasa limebadilishwa na kuwa afisi ya utalii

Habari hiyo iligonga vichwa vya habari nchini Cambodia ,ambapo ni zaidi ya asilimia 40 katika maeneo mashamabani walio na uwezo wa kwenda haja chooni.

Choo,hicho kilichojengwa ndani ya chumba kimoja kilicho na hewa safi kilijengwa kwa ziara ya binti mfalme huyo ya saa mbili.