Mbwa aliyepotea Uchina arudishwa na barua

Image caption Mbwa aliyeibwa Uchina

Mbwa mlinzi, ambaye alitekwa nyara na kusababisha hisia kali nchini Uchina amerudishwa kwa mwenyewe na barua ya kuomba msamaha, ripoti ya serikali imesema.

Qiaoqiao,aliripotiwa kuchukuliwa na kundi moja la wanaume Jumatatu , alipokuwa akipelekwa matembezi nje ya Ubelgiji.

Habari za mwenye mbwa aliyekuwa kipofu Tian Fengbo's na mbwa wake zilizua huzuni ambayo ilisababisha hasira miongoni mwa Wachina.

Mbwa huyo alipatikana Jumanne akiwa na barua kwenye mfuko wa plastiki katika shingo yake:

'tumekosea…tunaomba msamaha.'

Image caption Mbwa aliyepotea China

Bwana Tian amesema hangeweza 'kula au kulala' baaada ya Qiaoqiao, kupotea akiwa na miaka saba.

Wakaazi katika sehemu hiyo ambayo mbwa huyo aliibiwa,wameambia vyombo vya habari nchini humo kwamba kumekuwa na msururu wa uwizi wa mbwa.